Azam TV imeingia katika makubaliano na Chama cha Soka cha Kenya (Football_Kenya) kuonyesha Ligi Kuu ya FKF-pl kwa mkataba wenye thamani ya takriban Ksh300 milioni.

By Brian Magiri,31/8/2023

Azam TV imeingia katika makubaliano na Chama cha Soka cha Kenya (Football_Kenya) kuonyesha Ligi Kuu ya FKF-pl kwa mkataba wenye thamani ya takriban Ksh300 milioni ambao utaendelea kwa miaka 5 ijayo kuanzia sasa. Kwa mujibu wa takwimu rasmi kutoka @Football_Kenya, Azam TV italipa dola milioni 1 (sawa na Shilingi za Kenya 145,600,000) kwa msimu wa kwanza, na ongezeko la asilimia 10% kwa misimu saba inayofuata.
Azam TV imeeleza kuwa mechi za saa tisa alasiri zitaakuwa ugumu wa kuvutia watazamaji kwa hivyo wanapendelea nyakati zinazouza vizuri. Waliongeza na kusema kuwa timu kubwa zenye ufanisi na nchini ndizo Gor-mahia na AFC Leopards haziwezi cheza siku moja.
Rais wa shirikisho la kandanda nchini, Nick Mwendwa, amesema kuwa bado wanangojea makubaliano mengine na wathamini wengine hivyo hataweza kutangaza ni kiasi gani vilabu vitapokea kutoka kwenye makubaliano na Azam kwa sasa. Amesema itachukua takribani wiki moja hivi.