Rais William Ruto amesema hatavumilia kuona watu wachache wakiharibu mustakabali wa Wakenya.
By Brian Magiri, 31/8/2023,

Rais William Ruto amesema hatavumilia kuona watu wachache wakiharibu mustakabali wa Wakenya.”Biashara ya ufisadi lazima ifikie mwisho. Tutawashughulikia kwa nguvu,” Rais alisema.
Rais alisema kuwa maslahi ya ubinafsi ya baadhi ya viongozi serekalini yanakwamisha miradi ya maendeleo nchini. “Watu wachache hawawezi kutuzuia. Tutalipa gharama kuacha uovu huu,” aliongeza.
Rais Ruto aliwaonya wafisadi kwamba hawawezi tena kujificha mahakamani kwa amri za mahakama.”Tutafanya kazi kwa karibu na Mahakama ili kuwatokomeza wale wenye mtazamo wa kurudisha nyuma maendeleo,” alisema.
Kiongozi wa Nchi alikuwa akiongea Alhamisi katika upande Wa Magharibi Kaunti Ya Kakamega katika ziara yake ya siku tano ambapo alikutana na viongozi kutoka kaunti za Kisii, Nyamira, na Migori.
Viongozi walioadamana na Rais ni, Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu, Gavana Simba Arati (Kisii), Gavana Amos Nyaribo (Nyamira), pamoja na Wabunge, Wawakilishi Wadi na viongozi wa ngazi za chini.
Viongozi hao walikubaliana kufanya kazi na serikali katika kubadilisha Kenya, huku Rais akiwaomba viongozi kujitokeza zaidi ya maslahi finyu ya vyama vya kisiasa ambavyo vinaweza kudhoofisha maendeleo ya nchi.
