Kinara wa Azimio la Umoja akitoa hotuba yake katika ukumbi wa SKM September 16th 2023. Photo Courtesy

Raila alitangaza habari hiyo Jumamosi, Septemba 16, alipokuwa akizindua ripoti ya mwaka mmoja ya Rais Ruto, ambayo alidai mwaka mmoja umekuwa wakumfilishisha mwananchi wakawaida.

By Brian Magiri, sept 17th 2023.

Kiongozi wa Azimio La Umoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga amethibitisha kwamba yeye na muungano wake wa Azimio la Umoja wamekusanya zaidi ya sahihi milioni 10 huku wakiipa serikali ya Kenya Kwanza alama ya D- baada ya kutawala kwa mwaka mmoja.

Raila alitangaza habari hiyo Jumamosi, Septemba 16, alipokuwa akizindua ripoti ya mwaka mmoja ya Rais Ruto, ambayo alidai mwaka mmoja umekuwa wakumfilishisha mwananchi wakawaida.

Alieleza kuwa sahihi hizo zilikuwa ishara wazi kwamba Wakenya hawajaridhiki na serikali ya Ruto. Ingawa aliacha kufafanua jinsi atakavyotumia sahihi hizo alishinikiza Ruto kukubaliana na madai ya upinzani. Chama cha Azimio la Umoja One Kenya Coalition kilitaja mwaka wa kwanza wa utawala wa Rais William Ruto kuwa mwaka wa janga kwa Wakenya.

Kiongozi wa Upinzani alitoa asilimia 30 (D minus) kwa utawala wa sasa. “Kuna ahadi ambazo walitoa wakifanya kampeni. Hio Lugha imebadilika baada ya wao kushika hatamu ya utawala,” alisema. “Ripoti yetu kwa utawala huu ni asilimia 30, yaani D-.”alisema

Raila aliendelea kusema kuwa Wakenya watajiunga na maandamano tofauti sasa ikilinganishwa na awali .

Alisema, “Kama mnavyojua tumekuwa tunakusanya sahihi, kutoka kwa Wakenya. Sasa tumekusanya zaidi ya milioni kumi na sasa tumejua kile tutakachofanya na hizo sahihi.”

“Mara hii hatuwaambii raia warudi barabarani. Ikiwa watarudi, watarejea kwa sababu kabisa tofauti. Fuatilia nafasi hii!”

Raila alilaumu utawala wa Kenya Kwanza kwa kuingilia majukumu ya ugatuzi na kutumia vyombo vya serikali visivyofaa na kuashiria maandamano ya aina tofauti dhidi ya serikali